Alhamisi, 10 Januari 2013

SESEME HALOLE MWENYEWE

MTYARISHAJI:SHABANI ALLY SESEME

kutoka katika kitabu cha seseme halole mwenyewe

 MZEE MAHSEN (HUSSEIN HUSSEIN SESEME)   MAKUMBITU 1875- 1964.

Mzee Hussein Hussein Makumbitu ndiye kaka mkubwa wa wazee wetu hawa watatu wa ukoo huu wa Seseme. Wanandugu hao ni mzee Hussein Hussein mwenyewe, mzee Omar Hussein na mzee Abdallah Hussein Seseme. Baba yao ni mzee Hussein Abdallah na Babu yao ni mzee Abdallah (Seseme) Mzee wa ukoo huu.

Mzee Hussein Hussein kama watu walivyozoea kumwita, jina lake hasa ni Mahsen Hussein, hatunayo kumbukumbu nzuri sana ya mwaka na mahali hasa alipozaliwa. Lakini kama ilivyo kawaida yetu tunayo makisio tu ya umri wake aliofariki  tunahakika nao basi kwa kufanya mahesabu kidogo kumetupa mwaka          aliozaliwa ambao tunadhani kuwa umekaribiana sana na ukweli  kwa kuwa  Mwaka          aliozaliwa bila shaka 1875 hivi. Na kwa kuwa alifariki 1964 basi umri wake wa maisha ni kiasi cha miaka 89 (Themanini na tisa ) hivi alivyoishi.

Mama yao wazee wetu hawa ambaye ni mke wa mzee Hussein aliitwa Bi Mwafatima bint Mwinshehe kutoka Mlingotini Bagamoyo. Mzee HusseiAbdallah Seseme na mkewe Mwafatima binti Mwinshehe waliishi Mtoni kwa Azizi Ally  hadi mwisho wa maisha yao. Walipofariki wote wawili walizikwa hapo kwa Mtoni Sokoni

Hapo mwanzoni mwa maisha ya ndoa yake Mzee Hussein Abdallah Seseme na mkewe waliishi Mzizima eneo linaloitwa Malindi sasa ni Trafic Police

Jina la Hussein Hussein watu walilizoea kiurahisi sana kwa vile ilikuwa ni rahisi kwao kutamka Hussein kuliko Mahsen ambalo ndio jina lake halisi. Kwa hivyo kuita Mahsen Hussein ilipokuwa ikiwashinda watu kutamka ndipo wakarahisisha wakaita Hussein Hussein badala ya Mahsen Hussein.

Wasifu wake mzee Hussein Hussein alikuwa mtu wa miraba minne, nyusi nyingi kwenye kope za macho yake na paji la uso kwa jumla. Alionekana mtu aliyeshiba kimwili na mwenye nguvu nyingi na mcheshi lakini mkali kwa tabia. Mzee Hussein alikuwa hajizuii kumfokea mtu wa rika lolote popote pale iwapo ataona mtu huyo amekosa jambo Fulani la dhahiri. Hata hivyo alikuwa mtu wa harakati mwenye hekima, kupenda watu na maendeleo yao kwa jumla, hakupenda kumvunjia mtu heshima yake bila sababu. Hatukuwahi kusikia iwapo kama alikuwa mgomvi wa kupigana ngumi hovyo. Na wala kwa wazee wake ama vinginevyo. Pamoja na yote watu husema shina la mwiba huota mwiba kwa hivyo si ajabu pia ikiwa kama tabia hiyo ya mzeeHussein Hussein amerithi kutoka kwa mmoja wapo wa wazazi wake wawili, Baba au Mama.

Kutokana na muonekano wake huo, watani wake kwa maana ya watu kama  Wanyamwezi ama wajukuu walimpachika jina la utani “MAKUMBITU” hasa kutokana na hizo nyusi zake zilizojaa kwenye paji lake la uso, siyo siri alitisha kinamna yake hasa ukiwa na jambo unapotaka kumkabili kwa kutaka maelekezo kutoka kwake……
 INAENDELEA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni