Jumatano, 23 Januari 2013

WATOTO WA MZEE SESEME MAKUMBITU

MKE WA KWANZA WA MZEE HUSSEIN SESEME MAKUMBITU

Bi Chausiku Binti Mwanegoha  Kawambwa ndiye mke wake wa kwanza ambaye alizaa watoto wawili tu na kisha kufariki. Watoto hao ni mzee wetu Bw Athumani Hussein Seseme ambaye alimzaa mwaka 1922. Na mtoto wake wa pili ni mama yetu Bi Mwajuma binti Hussein Seseme ambaye alimzaa miaka miwili baadaye. Ama kati ya mwaka 1924 - 1925.Baadae Bi Chausiku alifariki dunia aliwaacha wanawe  Bw. Athumani na Bi. Mwajuma wangali wadogo bado. Bi Chausiku alizikwa kwa  Kombo pembeni mwa msikiti wa kwa Kombo mwaka 1926. Hivi hatuna tarehe yenyewe hasa.

MKE WA PILI WA MZEE HUSSEIN HUSSEIN (MAKUMBITU)

Bibi Khadija binti Salum Kiluke, kutoka Lukanga Mkuranga ndiye mke wa pili wa mzee Hussein Bi khedija alizaa na Mzee Hussein watoto wanane na alifariki 1980 watoto hao ni kama ifuatavyo.
    1 )   Bw. Muhamed Hussein alizaliwa mwaka 1928 alifariki 12/03/2004
     2)    Bw. Rajabu Hussein alizaliwa 1930 alifariki 16/01/2001
     3)    Bibi Mwajabu Hussein pacha na Bw. Rajabu alifariki julay 2004
     4)    Bw. Jaffar Hussein alizaliwa mwaka 1932 alifariki 06/01/2009
     5)    Bi Mwadawa Hussein alizaliwa mwaka 1938 alifariki
     6)    Bw. Mwinshehe Hussein alizaliwa 1941 bado yukohai
     7)    Bi Ashura Hussein alizaliwa mwaka 1943 alifariki march 2001
     8)    Bw. Ramadhani Hussein alizaliwa 1945 alifariki 2010.

MKE WA TATU WA MZEE HUSSEIN.

Mke wa tatu wa mzee Hussein ni bibi Tabu bint Salum kutoka Msanga ya Gumba Masaki Kisarawe, yeye amezaa watoto sita, bint Tabu ama (Heyaheya) alifariki tarehe 24/12/2000. Watoto hao ni kama ifuatavyo:-
1.    Bi Mwakama Hussein alizaliwa 1936 alifariki 14/12/2009
2.   Bw. Omari Hussein alizaliwa 1938 alifariki 1994
3.   Bi Kibibi Hussein alizaliwa 1940 alifariki December11,2011
4.    Bw. Ally Hussein alizaliwa mwaka 1942 yuko hai
5.   Bi. Husna Hussein alizaliwa mwaka 1944 yuko hai
6.   Bi Mariam Hussein alizaliwa mwaka 1947 yuko hai

MKE WA NNE WA MZEE HUSSEIN

Mke wa nne ni bibi binti Suleiman kutoka Kisarawe. Bibi huyu hakuzaa,alikuwa hana kizazi na alifariki mwaka 2004. Wakati wa kifo chake alikuwa ameshaachwa na mzee Hussein Hussein.
Kwa jumla Mzee Hussein Hussein alipata watoto kumi na sita (16) wanaume nane na wanawake nane. Waliofariki hadi kufikia wakati huu tunaandika kumbukumbu hii ni watoto kumi  na mbili (12).  Walio hai ni watoto wanne, wanaume wawili na wanawake wawili mpaka Mwezi Juni 2012.
JE UNAFAHAMU WEWE UMETOKANA NA KIZAZI KIPI KATI HAO?
endelea kufuatilia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni