Alhamisi, 10 Januari 2013

...............INAENDELEA....

Mzee Makumbitu na nduguze, inasemekana kuwa walisoma katika shule zilizoanzishwa na Wajerumani katika miaka ya 1894. Huenda ikawa Wajerumani walichangia kwa kiasi Fulani hii tabia ya ukali. Kwani Wajerumani japokuwa walikuwa watu rahimu sana hapo mwanzoni walipoingia Tanganyika na kujuana na wenyeji yaani Wazalendo lakini baadae walibadilika tabia wakaleta ile siasa ya kwao Ujerumani ambayo ni “HARSH MANAGEMENT AND HARSH DISCIPLINE” Kwa maana ya uongozi ulio na nidhamu, ngumu ngumu.Ngazi za shule hizo za Wajerumani zilikuwa tatu


Nebenschelen-Primary School

Haptoschulen-Middle School


Obenschulen-Shule ya kiufundi kwa vijana wenye umri mkubwa

Vile vile mzee Hussein na nduguze walisoma qur’ani na dini ya Kiislam, wakati wa utoto wao hakuna kumbukumbu ya hatua gani hasa walipofikia aidha kwenye dini, quraan na masomo ya kawaida kwenye shule za Kijerumani.

Inasemekana tu kuwa walisoma vyema na walifikia hatua ya kukubalika hususan katika wakati ule hadi kuaminika katika kazi za Kiserikali.

Na katika dini pia mzee Hussein Hussein alifikia daraja la kufungua madrasa yake mwenyewe hapo hapo Mtoni kwa Azizi Ally. Kwa hivyo alimudu kuwafundisha dini wenyeji hapo kwenye madrasa yake. Katika watu maarufu aliopata kuwafundisha inasemekana kuwa Sheikh Abdallah iddi Chaurembo ni mmojawapo, Bw Athumani Hussein, Bw Ramadhani Omari ni katika wanafunzi wake pia. Shekh Abdallah Iddi Chaurembo hatimaye alimuoa Bi Mwajuma Binti wa mzee Hussein Hussein Seseme Mwalimu wake. Mama huyo alizaa na Sheikh Chaurembo watoto wanne.

Bi Mwajuma alifariki Mnamo mwaka 1953.

Mzee Hussein Hussein alikuwa mtu wa harakati sana wakati wa uhai wake. Aliwahi kufanya kazi za kiserikali za chama cha TANU na hata kazi zake binafsi.
Mwaka 1945 wakati wa ukoloni wa Waingereza aliwahi kuwa mndewa (village cancellor) Mbagala na baadaye, Hakimu Vikindu kwenye mahakama ya kijiji Local Court mnamo mwaka 1950 kazi hizo alifanya hapo Vikindu .

Mwaka 1953 mahakama ilihamishiwa Mkuranga ndipo yeye alistaafu kazi hiyo
Mzee Hussein Hussein aliwahi kuoa wake wane ijapokuwa si wote kwa mara moja lakini alipata kukaa na wake watatu kwa mpigo. Na wake watatu ndio aliozaa nao isipokuwa mke mmoja binti Suleiman
ambaye hakuzaa, hakuwa na kizazi “mgumba”

ENDELEA KUFUATILIA HISTORIA YA MZEE MAKUMBITU

Maoni 2 :

  1. Baccarat Rules Explained - Worrione
    In most gambling sites, players have the 1xbet opportunity to หารายได้เสริม take To find 바카라 사이트 out which rules are applicable in the game of Baccarat, click here.

    JibuFuta